9.8 C
New York

Spika wa Bunge Ukraine auawa kwa kupigwa risasi

Published:

KYIV, Ukraine
ALIYEWAHI kuwa Mbunge nchini Ukraine, Andriy Parubiy, amefariki leo baada ya kupigwa risasi mjini Lviv, Ukraine.
Chanzo cha taarifa hiyo kimeeleza kuwa Parubiy alishambuliwa kwa risasi kadhaa na mtu asiyejulikana.
Parubiy aliyeiaga dunia akiwa na umri wa miaka 54, alikuwa mmoja ya wanasiasa waliokuwa wakimpinga Rais wa zamani, Viktor Yanukovych.
Kwa upande wake, Rais wa sasa, Volodymyr Zelensky, ameeleza kusikitishwa na kifo cha Parubiy akisema ni mauaji yasiyokubalika.
“Jitihada zote zinazowezekana zinahitajika kujua aliye nyuma ya mauaji haya,” alisema Zelensky.
Aidha, taarifa ya vyombo vya usalama vya Ukraine imedai kuwa vinaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo ili kubaini wahusika.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img