31.4 C
New York

Fei Toto apigwa bao ufungaji bora

Published:

Na Hassan Mwasha, Gazetini

NI rasmi sasa kiungo wa Azam, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amekikosa kiatu cha mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2025-26.

Fei Toto ameikosa tuzo hiyo baada ya mshambuliaji wa Singida Black Stars, Mossi Ndumumwe, kutupia ‘hat-trick’ katika mchezo wao dhidi ya Fountain Gate leo Juni 30, 2026.

Kabla ya mechi hiyo, Fei Toto ndiye aliyekuwa akiongoza kwenye mbio za ufungaji akiwa na mabao 15, wakati Mossi na Allan Okello wa Yanga walikuwa na 14 kila mmoja.

Hivyo, kwa hat-trick ya leo, Mossi amewapiga ba mastaa hao na kuwa mfungaji bora msimu huu wa Ligi kwa mabao yake 17.

Linaweza kuwa pigo kubwa kwa Fei Toto ambaye kwa muda mrefu ndiye aliyekuwa akiongoza kwenye mbio za kuwania kiatu.

Related articles

Recent articles