9.8 C
New York

Zelensky: Tutapigana na Urusi hadi kieleweke

Published:

KYIV, Ukraine
RAIS wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, amesema wataendeleza vita na Urusi hadi pale majirani zao hao watakapoacha kuwakandamiza.
Kauli ya Zelensky imekuja baada ya Urusi kudai kushambuliwa na Ukraine siku chache usiku wa jana.
Hata hivyo, Ukraine imekanusha vikali kuhusika katika mashambulizi hayo ya anga, ikisema ni kawaida ya Urusi kueneza propaganda.
“Tunachotaka ni amani, amani ya sisi wenyewe kuamua mambo yetu,” alisema Zelensky na kusisitiza kuwa Ukraine haitarudi nyuma katika mapambano ya kupigania uhuru wake.
Kwa upande mwingine, leo Urusi na Ukraine zimethibitisha kubadilishana wafungwa wa kijeshi takribani 146.
Zelensky amezungumzia wafungwa waliorejeshwa Ukraine kuwa ni pamoja na wanajeshi walioshikiliwa na Urusi tangu mwaka 2022.
Pia, alithibitisha kurudishwa kwa mwandishi wa habari, Dmytro Khilyuk, ambaye alikamatwa na wanajeshi wa Urusi wakati vita inaanza.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img