9.8 C
New York

Waasi 35 wauawa shambulizi la anga Nigeria

Published:

LAGOS, Nigeria

JESHI la Nigeria limedai kuua wapiganaji 35 wa moja ya vikundi vya waasi baada ya kufanya shambulizi la anga jirani na mpaka wa nchi hiyo na Cameroon.
Kwa mujibu wa taarifa yake, wapiganaji waliouawa ni wa kundi linalojinasibisha na Dini ya Uislam.
Kaskazini-Mashariki mwa Nigeria, jirani na mataifa ya Cameroon, Chad na Niger, kumekuwapo na matukio mengi ya waasi kushambulia makazi ya raia na hata kusababisha vifo na majeruhi.
Ni katika maeneo hayo, makundi ya Boko Haram na ‘Islamic State West Africa Province’ (ISWAP) yamekita mizizi na kuondosha hali ya usalama.
Kabla ya taarifa hii, tayari ilikuwepo ya wiki iliyopita, ikieleza kuwa jeshi limeua waasi 592 kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Vyanzo vya habari vinaeleza kuwa kukosekana kwa amani katika maeneo hayo kumesababisha watu zaidi ya milioni mbili kuyakimbia makazi yao.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img