9.3 C
New York

Usyk; mbabe wa ulingo, kiboko ya mabondia wa Uingereza

Published:

LOS ANGELES, Marekani
STAA wa ngumi za uzito wa juu, Oleksandr Usyk, ndiye bingwa wa dunia baada ya kumdunda kwa ‘KO’ ya raundi ya tano Daniel Dubois katika pambano la hivi karibuni.
Usyk, raia wa Ukraine mwenye umri wa miaka 38, ambaye hii ni mara yake ya pili kuwa bingwa wa dunia, alimchapa Dubois wa Uingereza, pambano likipigwa katika Uwanja wa Wembley jijini London.
Kabla ya kukutana na Usyk, Dubois alikuwa na rekodi ya kuvutia ya ushindi wa KO katika mapambano yake 24.
Ukiacha ubingwa mbele ya mashabiki 90,000, Usky ameendeleza rekodi yake nzuri kwenye masumbwi, likiwa ni pambano lake la 24 bila kupoteza.
Kwa upande mwingine, Dubois anakuwa bondia wa tatu wa Uingereza kupoteza mapambano yote mawili mbele ya Usyk baada ya wenzake wawili, Tyson Fury na Anthony Joshua.
Alipomchakaza Joshua na kutwaa ubingwa wa IBF mwishoni mwa mwaka jana, lilikuwa ni pambano lake la tatu tu tangu Usyk ajitose kwenye ulimwengu wa ngumi za uzito wa juu.
Kama itakumbukwa, ushindi wake dhidi ya Fury mwaka 2024, ulimfanya Usyk kuwa bingwa wa dunia akiwa na mikanda minne.
Sasa, baada ya Usky kuonekana tishio, huenda akakutana na bondia wa kiwango cha juu raia wa New Zealand, Joseph Parker.
Kwa miaka miwili ya hivi karibuni, Parker ambaye aliwahi kutwaa ubingwa wa WBO kwa kumdunda Andy Ruiz mwaka 2016, amewatandika Deontay Wilder, Zhilei Zhang na Martin Bakole.
Bondia huyo mwenye umri wa miaka 33, amepoteza mara tatu pekee katika mapambano yake 39, akishinda 24 kwa KO.
Hata hivyo, promota wa Parker, David Higgins, amekiri kulitamani pambano hilo, ingawa amesema hakuna mazungumzo yaliyofanyika.
Lakini pia, zipo taarifa zinazodai kuwa huenda Fury ambaye amestaafu, akarudi ulingoni na kurudiana na Usyk baada ya kudundwa mara zote mbili alizokutana na bondia huyo wa Ukraine.
Fury, kwa upande wake, amezipuuzia taarifa hizo na kudai kuwa bado hajafikiria kurejea kwenye masumbwi. “Kwa umri huu (miaka 36), sioni kama nitarudi. Ngumi ni mchezo wa vijana,” alisema.
Wakati akiendelea kuhusishwa na mabondia mbalimbali, Usyk amesema kwa sasa anafikiria zaidi kupata muda wa mapumziko. “Nataka kupumzika na familia, mke na watoto wangu. Nahitaji miezi miwili hadi mitatu,” alisisitiza Usyk.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img