12.5 C
New York

Chelsea wana nafasi ubingwa EPL 2025-26?

Published:

LONDON, England
BAADA ya kutwaa mataji ya Conference League, Chelsea walihitimisha furaha yao wikiendi iliyopita kwa kuifunga PSG mabao 3-0 na kubeba ubingwa wa Kombe la Dunia kwa ngazi ya Klabu.
Blues hawakuwa wakipewa nafasi kubwa ya kunyakua ‘ndoo’ hiyo, hasa baada ya
ya kufungwa mabao 3-1 na Flamengo katika mchezo wa hatua ya makundi.
Je, Blues wataingia na kasi hiyo msimu ujao wa Ligi Kuu ya England (EPL)? Nafasi yao ikoje kwenye mbio za ubingwa wa michuano hiyo?
UKAME WA MIAKA NANE
Ni miaka nane sasa imepita tangu Chelsea ilipobeba kwa mara ya mwisho ubingwa wa EPL. Ni tangu misimu wa 2016-17.
Tangu hapo, Blues wamekuwa nje ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, hadi walipokata tiketi ya michuano hiyo wiki ya mwisho ya msimu uliopita wakiwa wamezidiwa pointi 15 na mabingwa wa EPL, Liverpool.
Katika kujiweka sawa kwa ajili ya msimu ujao, kocha Enzo Maresca amekifanyia maboresho makubwa kikosi chake.
Katika maboresho hayo, Maresca amefanikiwa kuzinasa saini za Florian Wirtz, Jeremie Frimpong na Milos Kerkez.
Je, usajili huo utaizuia Liverpool kulitetea taji la EPL na kushuhudia safari hii likielekea Stamford Bridge?
Historia iko wazi, ikionesha kuwa Manchester City ndiyo timu pekee iliyoweza kutetea ubingwa huo tangu Manchester United ya Alex Ferguson ilipofanya hivyo mara mbili (2007-08 na 2008-09).
VITA YA LONDON
Chelsea hii itamaliza unyonge wake mbele ya wapinzani wao wa jijini London, Arsenal? Ni swali linalowasubiri vijana wa Maresca msimu ujao.
Kwa miaka ya hivi karibuni, Arsenal imekuwa ikiiacha mbali Chelsea, licha ya kwamba wenzao hao wa London nao hawajachukua ubingwa wa EPL tangu msimu wa 2003-04.
Msimu uliopita, Chelsea walizidiwa pointi tano na Arsenal kwenye msimamo wa EPL. Huo ukawa ni msimu wa pili mfululizo kwa Washika Bunduki kumaliza katika nafasi ya pili.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img