11.6 C
New York

Urusi yaiunga mkono Taliban

Published:

KYIV, Urusi
URUSI limekuwa taifa la kwanza kutangaza kuitambua Serikali ya Taliban inayoiongoza Afghanistan.
Haiishii hapo, bali pia Serikali ya Urusi kupitia kwa Wizara ya Mambo ya Nje imeahidi kuiunga mkono Taliban, hasa katika mapambano dhidi ya ugaidi na dawa za kulevya.
Taliban wanakumbana na ukosolewaji mkubwa, hasa kutoka kwa mataifa ya Magharibi, tangu walipoanza kuitawala Afghanistan miaka minne iliyopita.
Kupingwa kwa Taliban kunatokana na msimamo mkali, zikiwamo sheria zinazokandamiza wanawake.
Kwa upande wake, Serikali ya Taliban imekuwa ikipinga shutuma hizo, ikisisitiza kuwa si kwamba haiwaheshimu wanawake, bali inalinda utamaduni wa Afghanistan na sheria za Dini ya Uislam.
Aidha, taarifa za Urusi kuiunga mkono zimepokewa kwa furaha na Waziri wa Mambo ya Nje wa Afghanistan, Amir Khan Muttaqi, ambaye ameyataka mataifa mengine kuiga hatua hiyo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img