23.6 C
New York

Maajabu ya mfungwa mzee zaidi, aliwahi kutoroka gerezani

Published:

NEW YORK, Marekani

ANAITWA Francis Clifford Smith. Alipofariki Juni, 2026, alikuwa ndiye mfungwa mwenye umri mkubwa zaidi nchini Marekani. Miaka 101.

Smith alihukumiwa kwa makosa ya mauaji mwaka 1950, wakati huo akiwa kijana wa umri wa miaka 25 tu. Mara zote alisisitiza kuwa hakuwa na hatia.

Alihukumiwa kwa kosa la mwaka 1949, akitajwa kumpiga na kumsababishia kifo mlinzi wa ukumbi wa starehe aitwaye Grover Hart.

Hakuwa peke yake. Smith alikamatwa na mwenzake mmoja, wakihusishwa na mauaji hayo. Mwenzake aliachiwa baada ya kutoa ushahidi wa kuthibitisha kuwa Smith ndiye aliyeua.

Hata hivyo, bado ipo dhana kuwa Smith alikuwa sahihi mara zote. Kwamba hakuhusika katika mauaji hayo. Kwanini?

Mmoja ya maofisa wa upelelezi waliowahi kumuhoji, Leo Carroll, aliibuka miaka mingi baadaye na kusema: “Sina uhakika hata kama alikuwepo kwenye tukio.”

Mwaka 1954, hukumu yake ya kifo ilibadilishwa na kuwa kuifungo cha maisha gerezani. Hadi anafariki, alishakaa huko kwa miaka 76.

Mwaka 1967, Smith akiwa ameshaishi gerezani kwa miaka 16, alijaribu na kufanikiwa kutoroka gerezani lakini alikamatwa na kurejeshwa siku 12 tu baadaye.

Pia, zipo taarifa kuwa mwaka 1974 aliruhusiwa kurudi nyumbani kusherehekea Sikukuu ya Krismasi (Desemba 25), kisha kurudi gerezani siku iliyofuata.

Mwaka 1975, alipewa msamaha wa rais lakini alikaa uraiani kwa miezi 10 tu, kabla ya kurudishwa kwa kosa la kukiuka masharti ya msamaha. Alikutwa na silaha.

Tangu hapo, Smith aliendelea kusota kwenye kuta za gereza hadi alipofikwa na umauti miezi miwili iliyopita akiwa na umri wa miaka 101.

Kwa kipindi chote cha maisha yake ya gerezani, Smith alijizolea umaarufu mkubwa kwa tabia yake ya kula ndege, kiasi cha kupewa jina la ‘Birdman’ na wafungwa wenzake.

Aidha, takwimu za Marekani za mwaka 2025 zinaonesha kuwa idadi ya wafungwa wenye umri kuanzia miaka 55 na kuendelea imeongezeka kwa asilimia 400 kuanzia mwaka 1991 hadi mwaka 2021.

Related articles

Recent articles