MADRID, Hispania
KIUNGO wa zamani wa Arsenal, Santi Cazorla, anaamini winga wa Barcelona, Lamine Yamal, ana kila sababu ya kutwaa tuzo ya mwaka huu ya Ballon d’Or.
Cazorla amesisitiza kuwa Mhispania mwenzake huyo mwenye umri wa miaka 19 ana haki zote za kuwa mshindi wa tuzo hiyo ya Mchezaji Bora wa Mwaka.
Akihojiwa na kituo cha televisheni cha SPORT, Cazorla amesema: “Ningempa Lamine tuzo ya Ballon d’Or.
“Anacheza timu yetu ya Taifa, ni Mhispania na ana haki zote za kushinda tuzo,” amesema Cazorla, ambaye pia aliwahi kuitumikia Hispania katika ngazi ya timu ya taifa.
Kwa upande wake, Yamal anakabiliwa na upinzani mkali wa kuipata tuzo hiyo mbele ya Harry Kane wa Bayern Munich na staa wa Real Madrid, Kylian Mbappe.


