16.9 C
New York

Kolabo ya Mr. Eazi, Moliy heshima zaidi!

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

STAA wa muziki wa Afropop Mr. Eazi hajawatelekeza mashabiki zake, kwani amerudi na wimbo mpya uitwao Comfort.

Ngoma hii kali yenye mahadhi ha Afo Pop, amemshirikisha mwanamuziki kutoka Ghana, Moliy anayefahamika kujitengenezea umalkia wake kwenye kibao ‘ Shake it To The Max’.

Comfort ni wimbo wa kujisikia vizuri unaochanganya sauti ya kipekee ya Mr. Eazi ya Banku Music na sauti tamu ya Moliy, ukiupatia wimbo huo hisia freshi na ya kuchekesha.

Kazi hiyo imepitia kwenye mikono iliyobarikiwa ya Ragee, mtayarishaji maarufu wa Nigeria nyuma ya hit za hivi karibuni za Davido (Unavailable) na Ayra Starr (Hot Body, Who’s Dat Girl.

Comfort inachanganya Afrobeats, Dancehall na R&B kwa mdundo wa kustarehesha na melodi inayoshika, ukiwapa Mr. Eazi na Moliy nafasi ya kuonesha vipaji vyao huku wakileta nguvu ya kustarehe na mahaba kwenye wimbo huo.

Akizungumzia wimbo huo, Mr. Eazi anasema: “Hii ni toleo lililoboreshwa la sauti yangu ya kipekee. Ninatengeneza muziki wa kina dada, muziki mtamu, mwepesi, unaowasifia kina dada. Ni kuhusu kuweka mambo mepesi, ya kufurahisha na yanayokufanya ujisikie vizuri, huku bado nikiwapa watu sauti ile ile ya Mr Eazi wanayoijua na kuipenda.”

“Comfort” unakaa vyema kwenye makutano ya aina za muziki zilizounda sauti ya Banku Music ya Mr Eazi.

Pini hiyo imekuja katika kipindi cha mafanikio ya muziki mpya kutoka kwa Mr Eazi mwaka 2026.

Mapema mwaka huu Me. Eazi, aliungana na mtayarishaji wa Dancehall wa Marekani Dre Skull kwa mfululizo wa nyimbo zikiwemo “Lambo” akiwa na Vybz Kartel, “Hide Your Love” na “Remember That,” akiwa na gwiji wa dancehall Cham.

https://empawaafrica.lnk.to/MrEaziComfort

Related articles

Recent articles