ROMA, Italia
ZIPO taarifa zinazodai kuwa klabu ya AS Roma iko mbioni kumchukua beki aliyeachana na Bayern Munich, Raphael Guerreiro.
Kwa mujibu wa ripoti, kocha wa timu hiyo ya Ligi Kuu ya Italia [Serie A], Gian Piero Gasperini, ndiye anayemtaka nyota huyo.
Nyota huyo raia wa Ureno hana timu kwa sasa, hivyo kanuni zinamruhusu kusajiliwa, licha ya kufungwa kwa dirisha la usajili.
Mwanzoni mwa dirisha la kiangazi, 2026, Guerreiro alikuwa akihusishwa na klabu za AC Milan na Bayer Leverkusen lakini hakuna dili lililokamilika.
Guerreiro alicheza mechi 95 akiwa na Bayern, ambapo aliweza kufunga mabao 14 na kutoa ‘asisti’ nane.


