15.3 C
New York

Sabalenka ang’olewa China Open

Published:

BEIJING, China

LICHA ya kushika nafasi ya pili katika viwango vya ubora duniani, staa wa tenesi, Aryna Sabalenka, amejikuta akitolewa kwenye michuano ya China Open.

Hii inakuwa mara ya pili tangu mwaka 2015 kwa mchezaji anayeshika nafasi ya pili duniani kushindwa kuingia hatua ya 16 Bora ya China Open.

Safari yake kwenye mashindano hayo imekwamishwa na Nikola Bartunkova ambaye anashika nafasi ya 34 duniani.

Katika mchezo huo, Bartunkova raia wa Jamhuri ya Czech alimduwaza Sabalenka kwa ushindi wa seti 6-4 6-3.

Baada ya mechi hiyo, Bartunkova amesema haikuwa rahisi kumshinda nyota huyo, hasa kutokana na uzoefu wake kwenye mchezo wa tenesi. “Ni mkongwe, kwa hiyo nimefurahi sana kushinda mechi hii.”

Related articles

Recent articles