PRETORIA, Afrika Kusini
LICHA ya kuiwezesha timu ya soka ya Taifa ya Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’ kufika hatua ya mtoano katika fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu (2026), kocha Hugo Broos ameachia ngazi.
Aliyetangaza kuondoka kwa Bross jana Julai 31, 2026 ni Rais wa Chama cha Soka cha Afrika Kusini (SAFA), Danny Jordaan. Kocha huyo ameondoka akiwa amemaliza mkataba.
Aidha, Bross mwenye umri wa miaka 74 ameliacha benchi la ufundi akiwa ameinoa Bafana Bafana kwa miaka mitano.
Raia huyo wa Ubelgiji alikabidhiwa mikoba mwaka 2019 baada ya timu hiyo kushindwa kufuzu fainali za Mataifa Afrika (AFCON) za mwaka 2021.
Chini yake, Bafana Bafana ilifuzu fainali zilizofuta za AFCON 2023 na timu hiyo kufika nusu fainali na kushika nafasi ya tatu.
Bross ameiongoza Bafana Bafana katika michezo 60 ya michuano mbalimbali. Kati ya hizo, ameshinda 29 (46.2%), sare 19 na kufungwa 12.


