26 C
New York

Utafiti: Ugumu wa maisha huathiri ubongo

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

NI utafiti uliofanywa na wanasayansi nchini Uingereza, ukibaini kuwa changamoto za kiuchumi zina athari kubwa katika afya ya ubongo.

Utafiti huo umefanywa kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Michigan na kuchapishwa katika jarida maarufu la Innovation in Aging.

Kwa mujibu wa ufafiti huo, wanasayansi walitumia ‘sampo’ ya watu 2,700 waliozaliwa Machi, 1946.

Baada ya miaka kadhaa ya wanasayansi kufuatilia afya za watu hao, walibaini kuwa asilimia 20 walikuwa na maisha magumu ya kipato wakati wa ujana wao.

Hivyo, wakiwa na umri wa miaka 80 kwa sasa, watu hao walibainika kupitia changamoto ya afya ya ubongo, ikiwamo kupoteza kumbukumbu.

Majibu hayo yalitokana na vipimo, pamoja na mazoezi madogo ya kusoma na kuhesabu haraka haraka.

Jacques Wels, mmoja ya watafiti wa Chuo Kikuu cha Michigan, ambaye pia ameshiriki katika utafiti huo, amesema: “Ni kwa sababu mzigo wa mawazo ya kiuchumi inachukua nafasi kubwa katika ubongo.”

Related articles

Recent articles