26 C
New York

Familia inayomlilia mwanasiasa wa upinzani anayesota gerezani

Published:

TUNIS, Tunisia

BADO hakuna taarifa rasmi za mamlaka juu ya anakotibiwa mwanasiasa maarufu wa upinzani nchini Tunisia, Rached Ghannouchi.

Wapo wanaosema yuko hospitali ya umma na wengine wanadai alipelekwa hospitali ya jeshi. Serikali haijathibitisha wala kukanusha taarifa yoyote kati ya hizo. Ipo kimya.

Kwa mujibu wa mtoto wake wa kiume, Moadh Ghannouchi, familia na wanasheria wake wamezuiwa kwa siku zaidi ya 10 kumuona
Ghannouchi mwenye umri wa miaka 81.

Ghannouchi aliyewahi kuwa Spika wa Bunge, anatumikia kifungo cha maisha kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kuchochea vurugu na chuki dhidi ya Serikali ya Rais Kais Saied. Alihukumiwa mwaka 2023.

Hivi karibuni, ziliibuka taarifa za kukimbizwa hospitali baada ya melazwa hospitali baada ya kuanguka akiwa gerezani, kwa mujibu wa Moadh.

Moadh ameeleza kuwa mara ya mwisho kumuona mzee wao huyo ilikuwa Julai 17, 2026, yaani kabla ya tukio hilo la kupelekwa hospitali.

Kwa mujibu wake, walituma barua kwa mwendesha mashitaka wakiomba kuruhusiwa kwenda hospitali lakini wamekataliwa.

Anaweza kuwa kunyimwa ruhusa, pia kutokuwa na taarifa juu ya aliko na hali yake vimeifanya familia ibaki sintofahamu na huzuni kubwa. “Ni kama amepotezwa,” anasema Moadh.

Aidha, anaongeza kuwa baba yake alikuwa na changamoto za kiafya, ikiwamo shinikizo la damu na shida ya kupumua, lakini amewekwa kwenye chumba cha gereza chenye joto bila kiyoyozi (AC).

Madai hayo yanaungwa mkono na Haifa Chebii, binti wa mmoja ya wafungwa katika Gereza hilo la Mornaguia, akisema Ghannouchi alipoteza fahamu baada ya kuzidiwa na joto kali.

Hivyo, Moadh anasema: “Mamlaka zinawajibika kwa hali yake hiyo. Mazingira magumu hayo yamelenga kudhohofisha afya ya baba yake. Kumfunga haijatosha, wanataka ateseke zaidi.

“Inatutesa na kumtesa pia. Alizoea kutembelewa na watu wengi, wanasheria na familia yake. Ni siku 11 sasa bila chochote, bila kutembelewa, bila kumuona yeyote.”

Katika hatua nyingine, Umoja wa Mataifa (UN) ulishawahi kutoa maelekezo ya kuachiwa kwa Ghannouchi kwa maelezo kwamba kesi yake ni ya kisiasa.

Na siku chache zilizopita, Umoja wa vyama vya siasa vya upinzani nchini Tunisia vilitoa tamko la kutaka Serikali itoe taarifa juu ya hali ya kiafya ya mwenzao huo.

Related articles

Recent articles