29.1 C
New York

Marekani, Iran zatulia; bei ya mafuta yashuka

Published:

WASHINGTON DC, Marekani

BEI ya mafuta katika soko la dunia imeshuka kwa asilimia 9, yakiwa ni matokeo ya mashambulizi ya Marekani na Iran kusimamia kwa siku mbili.

Kwa sasa, bei ya pipa moja la mafuta ghafi imefikia Dola za Marekani 88, tofauti na zaidi ya Dola 100 wiki iliyopita.

Hatua hiyo inakuja baada ya balozi wa Marekani ndani ya UN kusema mashambulizi kati nchi hiyo na Iran yamesimama kwa siku mbili mfululizo.

Kwa kipindi chote cha vita vilivyoanza Februari 28, 2026, bei ya mafuta duniani imekuwa haitabiriki, mara nyingi ikionekana kupanda.

Kupanda huko kumekuwa kukisababishwa na mapigano hayo kuugusa Mlango-Bahari wa Hormuz, ambao hupitisha meli zinazobeba asilimia 20 ya mafuta na gesi asilia zinazoingia kwenye soko la dunia.

Related articles

Recent articles