28.2 C
New York

Hezbollah waionya Serikali ya Lebanon

Published:

BEIRUT, Lebanon

KUNDI linalohusishwa na ugaidi la Hezbollah limeionya Serikali ya Lebanon, likisema inaipeleka pabaya nchi hiyo ya Mashariki ya Kati.

Mbunge mwandamizi wa Hezbollah, Ali Fayyad, amesema hayo akieleza kutokufurahishwa na hatua ya Serikali kukaa mezani na Israel.

Fayyad ameeleza kuwa Serikali ya Lebanon inataka maridhiano na Israel kana kwamba haioni uharibifu mkubwa uliofanywa na Taifa hilo nchini kwao.

“Ni kama hakuna kilichotokea,” amesema Fayyad, akilenga hatua ya Israel kuteka eneo lote la Kusini mwa Lebanon.

“Inaonekana wazi kwamba mamlaka zimepuuza watu wake na hazioni uhalifu mkubwa uliofanywa na Israel,” amesisitiza.

Kwa mujibu wa Fayyad, kukaa mezani na Israel ni kuhalalisha Lebanon iendelee kuwa chini ya udhalimu wa Israel na washirika wake, Marekani.

Related articles

Recent articles