WASHINGTON DC, Marekani
RAIS Donald Trump ameibuka na madai kuwa wapinzani wao wakubwa kiuchumi, China, walitia mkono katika Uchaguzi Mkuu wa Marekani wa mwaka 2020.
Kwa mujibu wa Rais Trump, China iliweza kunasa rekodi za wapiga kura zaidi ya milioni 220 kuelekea Uchaguzi Mkuu huo aliopoteza mbele ya Joe Biden.
Kauli hiyo ameitoa leo Julai 17, 2026, katika Mkutano wake na waandishi wa habari Ikulu mjini Washington DC.
Kwa mujibu wake, aliibiwa ushindi kwa ushirikiano kati ya China na timu ya kampeni ya Biden.
Katika hotuba yake, ameahidi kuagiza uchunguzi ufanyike, ingawa hakueleza ni kwa namna gani China iliwezesha Biden kushinda baada ya kupata takwimu za wapiga kura.
Hata hivyo, wakosoaji wake wanasema Rais Trump anajihami akifahamu wazi kuwa Chama chake cha Republican hakitofanya vizuri katika Uchaguzi mdogo ujao wa Novemba, 2026.


