30.3 C
New York

Video ya Diamond yazua gumzo hatima ya Zuchu

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

SIKU chache tu baada ya taarifa za Diamond Platnumz kuachana na Zuchu, imeibuka video ya bosi huyo wa Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) na kuzua taharuki.

Iko hivi; Zuchu ndiye aliyekuwa wa kwanza kutangaza mitandaoni kuwa ameachana na Diamond baada ya kipindi kisichozidi cha mwaka mmoja wa ndoa yao.

Sasa, baada ya Zuchu kuweka wazi kuwa mlolongo wa talaka unaendelea, imeibuka video ya Diamond akisema mali zake zote ameziandikisha kwa jina la mama yake.

Video hiyo ni ya zamani na ilirekodiwa katika moja ya sherehe za ‘birthday’ ya mama yake. Mali hizo ni pamoja na magari, nyumba na biashara zake.

Hata hivyo, video hiyo kwa sasa inatoa picha ya wasiwasi juu ya hatima ya Zuchu katika mali alizotarajiwa kupata baada ya kuachana na supastaa huyo wa Bongo Fleva.

Related articles

Recent articles