30.3 C
New York

Iran inatishia au italipiza kisasi kifo cha Khamenei?

Published:

TEHRAN, Iran

TANGU Iran ilipomzika Ayatollah Ali Khamenei siku chache zilizopita, mamlaka za nchi hiyo zimeahidi kulipiza kisasi kwa wahusika wa mauaji ya kiongozi wao huyo.

Mtoto wake, Mojtaba Khamenei, ambaye ndiye kiongozi aliyechukua nafasi ya baba yake, alisema: “Tunaapa kulipiza kisasi kwa ajili ya damu yako safi …”

Si tu kiongozi huyo, bali pia wanasiasa na vyombo vya habari vya umma nchini Iran wamekuwa na mtazamo huo, kwamba lazima walipize kisasi kwa ajili ya Khamenei.

Julai 14, 2026, kikao cha kwanza cha Bunge tangu vita dhidi ya Marekani vilipoanza Februari 28 kilishuhudia wabunge wakituma ujumbe wa kutaka kisasi.

Wabunge zaidi ya 180 kati ya 290 walitoa maoni yao yenye mlengo huo wa kutaka damu ya kiongozi wao isiende bila wahusika kushughulikiwa.

Katika hatua nyingine, Gazeti la Hamshahri lilichapisha orodha ya majina ya wanaopaswa kusakwa na kuuawa, kama sehemu ya kisasi hicho.

Orodha hiyo ilijumuhisha wanasiasa 13 wa nchi za Magharibi, viongozi wa kijeshi, mawaziri wa mambo ya nje na ulinzi, pamoja na Kansela wa Ujerumani, Friedrich Merz.

Hilo lilionekana wazi baada ya kifo cha Seneta wa Marekani, Lindsey Graham, ambapo Iran ilieleza kufurahishwa nazo, ingawa haikuhusika kumuua.

Graham alifahamika kwa ukaribu wake na Rais Donald Trump, pia akiunga mkono hatua ngumu za Marekani dhidi ya Iran, yakiwamo mashambulizi ya kijeshi.

Hata hivyo, kwa baadhi ya wachambuzi, vitisho hivyo havina maana yoyote zaidi ya Iran kujaribu kujipoza kisaikolojia baada ya pigo zito la kumpoteza Khamenei.

Kwa upande wake, mwanasheria ambaye pia ni mtafiti wa haki za binadamu, Moein Khazaeli, anaiona Iran ikijaribu kuilaghai dunia.

Kwamba vitisho hivyo vinalenga kujitutumua mbele ya wapinzani wake, kuonesha kuwa bado ina nguvu ya kijeshi, licha ya kiongozi wao huyo kuuawa.

“Kwa miaka mingi, Dola ya Kiislam (Iran) imekuwa ikitumia vitisho kama njia ya kupoza kushindwa kwao kijeshi au kiusalama,” amesema Khazaeli.

Aidha, Khazaeli amesema ujumbe huo unalenga pia kuwatisha waandishi wa habari, wanaharakati wa kisiasa, watetezi wa haki za binadamu waliopo nchini Iran.

Related articles

Recent articles