31.3 C
New York

Geita Gold ilivyovunja rekodi ikitinga tena Ligi Kuu Bara

Published:

Na Hassan Mwasha, Gazetini

GEITA Gold haijatinga Ligi Kuu Bara kinyonge, na badala yake imetwaa ubingwa wa Ligi Daraja la Kwanza Bara (Championship) ikiwa na pointi 77.

Idadi hiyo ni kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa kwa timu iliyotwaa ubingwa wa Championship kwa misimu mitatu ya hivi karibuni.

Msimu uliopita, 2024-25, Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro ndiyo iliyokuwa bingwa baada ya kukusanya pointi 71 katika michezo 30.

Pia, idadi ya pointi 77 za Geita Gold haikufikiwa na KenGold iliyokuwa bingwa wa msimu wa nyuma yake, 2023-24.

Katika msimu huo, KenGold ilitwaa taji la Championship ikiwa na jumla ya pointi 70 pekee.

Related articles

Recent articles