30 C
New York

Baba yake Kim Kardashian alivyobadili jinsia na kuwa mwanamke

Published:

LOS ANGELES, Marekani

OKTOBA 28,1976, dunia ilikuwa ikimtazama mwanaume aitwaye Bruce Jenner akitwaa medali ya dhahabu katika michuano ya Olimipiki kwa upande wa mchezo wenye mchanganyiko wa kukimbia, kuruka na kurusha vitu.

Baada ya ubingwa huo, jina la Jenner likawa maarufu na hata kupata dili nyingi za uchambuzi wa mchezo huo kwenye runinga, matangazo na kuchapisha vitabu vilivyouza nakala nyingi ndani na nje ya Marekani.

Mwaka 1991, Jenner alifunga ndoa na mrembo aitwaye Kris Kardashian ambaye alitoka kuachana na mwanasheria Robert Kardashian aliyezaa naye watoto wanne; Kourtney, Kim, Khloe na Robert.

Ukiachilia mbali ustaa wa Jenner baada ya ubingwa wa Olimipiki, ‘kapo’ yake na Kris ilipata umaarufu zaidi kupitia kipindi chao cha runinga cha ‘Keeping Up with the Kardashians’ kilichoanza kuruka hewani mwaka 2007.

Hata hivyo, ndoa yao iliyobahatika kupata watoto wawili – Kendall na Kylie – ilivunjika mwaka 2014.

ATUMBUI JIPU, ASEMA ALITAMANI KITAMBO

Aprili, 2015, miezi kadhaa baada ya kuachana na mke wake wa pili, Linda Thompson, Jenner aliitikisa dunia kwa mara nyingine.

Safari hii haikuwa ishu ya Olimipiki wala kurudiana na Kris, bali kujitangaza kuwa ni mwanamke na kutaka aanze kuitwa Caitlyn Jenner.

“Watu wananiona tofauti. Wananiona kama mwanaume … Mimi ni mwanamke. Ndivyo nilivyo,” alisema Jenner katika mahojiano yake ya wakati huo.

Jenner alisema hakukurupuka, bali ni kwa muda mrefu, tangu akiwa mdogo, alitamani kuwa mwanamke na si mwanaume.

Alisema: “Nilianza kujiona kwenye sura ya mwanamke tangu nikiwa na umri wa miaka nane au tisa. Nilikuwa nikijaribu mavazi ya mama au dada zangu.”

Aliongeza kuwa hata akiwa staa, alivaa nguo za kike kwa siri akiwa kwenye vyumba vya hoteli alizokuwa akifikia.

“Nilikuwa nikiingia chumbani, navaa nguo za kike, kisha naanza kutembea kama mwanamke,” alisema.

Alisisitiza kuwa ilikuwa ni ndoto yake ya muda mrefu kuishi kama mwanamke, lakini hakutaka kufichua mapema, akisubiri watoto wake wakue na kuanza kujitegemea, ndipo aanike ukweli wa mambo.

Anasema siku alipoamua kufichua ukweli, aliwaita watoto wake wote 10, pamoja na mama yake mzazi. “Walilia, hawakutaka kunikosea. Mara zote wamekuwa wakinilinda,” alisema.

WATOTO WAKE WAFUNGUKA

Jenner, mbali ya watoto wake sita, pia ana wanne aliowasili; Burt, Cassandra, Brandon na Brody.

“Ni heshima na najivunia mno kuwa kwenye familia hii,” alisema Brandon alipoulizwa kama anajisikia aibu kuwa na baba aina ya Jenner.

Kwa upande wake, Kim, ambaye ni ‘mtoto wa kambo’ katika ndoa yake na Kris, alisema: “Familia inajivunia kuwa naye.”

APEWA TUZO ‘MALKIA WA NGUVU’

Ilikuwa ni Agosti, 2015, ambapo Jenner alitwaa tuzo ya ‘Malkia wa Mitandao ya Kijamii’ katika tuzo za ‘Teen Choice Awards’. Mwezi huo pia, alibeba tuzo ya ‘Mwanamke Bora wa Mwaka’.

Mwaka huo huo, Jenner alitajwa kuwa ndiye mtu aliyetafutwa zaidi kwa upande wa Google. Mwaka 2016, Jarida la Times lilimtaja katika orodha ya watu 100 wenye ushawishi zaidi duniani.

Related articles

Recent articles