24.5 C
New York

Mastaa wa soka wenye elimu kubwa duniani

Published:

LONDON, Uingereza

KIUNGO wa zamani wa klabu za Valencia, Manchester United na Chelsea, Juan Mara, yumo kwenye orodha hii, akiwa na Shahada (Digrii) mbili.

Digrii yake ya kwanza ni ya Masomo, kabla ya kuchukua nyingine ya Sayansi ya Michezo katika Chuo Kikuu cha Jose Cela mjini Madrid, Hispania.

Kocha wa Bayern Munich, Vincent Kompany, naye ni miongoni mwa wanasoka wenye elimu zao. Beki huyo wa zamani wa Manchester City ana Shahada ya Uzamili (Master’degree) ya Usimamizi wa Biashara (Business Administration) kutoka Chuo Kikuu cha Alliance Manchester.

Ukiacha hao, yumo pia mlinzi wa kati wa zamani wa timu ya Taifa ya Italia, Giorgio Chiellini, ambaye ana Digrii ya Uchumi na Biashara.

Pia, Chiellini aliyewahi kukipiga Juventus ana Shahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Biashara aliyotunukiwa na Chuo Kikuu cha Turin, Italia.

Kiungo wa zamani wa Barcelona na timu ya Taifa ya Hispania, Andres Iniesta, naye ana Digrii ya Baiolojia kutoka Chuo Kikuu cha Castilla-La Mancha.

Wakati huo huo, yumo pia kipa wa kimataifa wa Ubelgiji, Simon Mignolet. Nyota huyo wa zamani wa Liverpool ana Digrii ya Sayansi ya Siasa kutoka Chuo Kikuu cha Leuven nchini Ubelgiji.

Unamkumbuka beki wa zamani wa Liverpool na timu ya Taifa ya England, Glen Johnson? Nyota huyo naye ni msomi mwenye Digrii ya Hisabati.

Related articles

Recent articles