MEXICO CITY, Mexico
WINGA wa timu ya Taifa ya Brazil, Vinicius, amesema sare ya bao 1-1 waliyopata katika mchezo wa kwanza dhidi ya Morocco umewapa somo na sasa wanajipanga kwa ajili ya mechi ijayo.
Katika mchezo huo wa kwanza kwa timu zote msimu huu wa Kombe la Dunia, Morocco walitangulia kupata bao kupitia kwa Ismael Saibari, kabla ya Vinicius kuisawazishia Brazil.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Vinicus ameandika: “Asante Mungu, tunataka kuimarika zaidi. Twende pamoja Brazil.”
Brazil watarejea uwanjani Juni 19, 2026 kwa mchezo wao wa pili dhidi ya Haiti waliotoka kufungwa bao 1-0 na Scotland.
Baada ya mtanange huo, vijana hao wa kocha Carlo Ancelotti watarudi mzigoni Juni 24, 2026, ambapo watavaana na Scotland katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi.


