24.5 C
New York

Ujerumani yaweka rekodi mpya Kombe la Dunia

Published:

NEW YORK, Ujerumani

BAADA ya ushindi wa mabao 7-1 dhidi ya Curacao, timu ya soka ya Taifa ya Ujerumani imeandika historia mpya katika michuano ya Kombe la Dunia tangu ilipoanzishwa mwaka 1930.

Katika mchezo huo wa Kundi C, Ujerumani ilipata mabao yake kupitia Kai Havertz (mawili), Felix Nmecha, Nico Schlotterbeck, Jamal Musiala, Nathaniel Brown, na Denis Undav.

Kwa ushindi huo, Ujerumani imefikisha mabao 239 katika historia ya mashindano hayo ya FIFA (Shirikisho la Soka la Kimataifa).

Hivyo, Ujerumani inaizidi Brazil bao moja. Selecao wanaweza kuwafikia endapo wataifunga Haiti katika mchezo wa Ijumaa ya wiki hii.

Ujerumani watarudi dimbani siku inayofuata, ambapo watakuwa na kibarua kigumu mbele ya Ivory Coast.

Related articles

Recent articles