NEW YORK, Marekani
KATIKA ripoti yake ya hivi karibuni, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) limeeleza kuwa watu milioni 118 walikimbia makazi au nchi zao kufikia mwishoni mwa mwaka 2025.
Aidha, ripoti hiyo ya UNHCR imetaja baadhi ya sababu hizo kuwa ni vita na kuomba hifadhi au uangalizi wa kimataifa, huku asilimia 39 wakiwa ni watoto.
Wakati huo huo, imeonesha kuwa nchi za Colombia, Ujerumani na Uturuki ndizo zilizopokea idadi kubwa ya wakimbizi mwaka 2025, zaidi ya milioni mbili kila moja.
Kwa upande mwingine, ripoti imeeleza kuwa nchi tatu – Syria, Afghanistan na Sudan – zilishuhudia asilimia 90 ya wakimbizi wake wa nje wakirejea nyumbani mwaka 2025.


