ZAPOPAN, Mexico
TIMU ya soka ya Taifa ya Korea ya Kusini imepata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Jamhuri ya Czech katika mchezo wa alfajiri ya leo Juni 12, 2026 uliochezwa kwenye Uwanja wa Guadalajara.
Bao la dakika ya 80 la Oh Hyeon-gyu aliyetokea benchi ndilo lililoipa Korea pointi tatu muhimu katika mchezo huo wa Kundi A baada ya kuingia uwanjani na kukuta sare ya bao 1-1.
Czech walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Ladislav Krejci aliyefunga kwa kichwa dakika ya 59, kabla ya Hwang In-beom kusawazisha dakika nane tu baadaye.
REKODI YAWEKWA
Hiyo imekuwa mara ya nne kwa Korea ya Kusini kushinda mchezo wa ufunguzi katika historia ya Kombe la Dunia baada ya kufanya hivyo mwaka 2002, 2006 na 2010.
Hata hivyo, ni mara moja pekee kwa Taifa hilo la Mashariki mwa Ulaya ilishindwa kuvuka hatua ya makundi. Ni mwaka 2006.
KITUO KINACHOFUATA
Mechi ya Kundi A inayofuata kwa Korea ya Kusini ni dhidi ya wenyeji wa michuano hiyo, Mexico. Medhi itachezwa Alhamisi ya wiki ijayo mjini Guadalajara.
Kwa upande wao, Czech watarudi dimbani Juni 18, 2026 kuvaana na Afrika ya Kusini ‘Bafana Bafana’ ambao nao walipoteza mechi yao ya kwanza dhidi ya Mexico.


