33.3 C
New York

UEFA yamkabidhi PSG refa aliyebaniwa Kombe la Dunia

Published:

MOGADISHU, Somalia

ZIKIWA ni siku chache tu tangu alipozuiwa kuingia Marekani, hivyo kukosa nafasi ya kuchezesha Kombe la Dunia, mwamuzi raia wa Somalia, Omar Artan, amepata dili jingine kutoka Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA).

UEFA imemkabidhi refa huyo mchezo wa Super Cup utakaozikutanisha bingwa wa Ligi ya Mabingwa, PSG, na mbabe wa Ligi ya Europa, Aston Villa. Mechi itachezwa Agosti 12, 2026 mjini Salzburg.

Kwa mujibu wa UEFA, uamuzi huo umekuja baada ya kuwasiliana na kufanya mazungumzo na Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF).

Artan alizuiwa akiwa Miami, Marekani, ikielezwa kuwa maofisa wa uhamiaji wa nchi hiyo walimtaka kurudi nyumbani baada ya kufanya naye mahojiano.

Kwa mujibu wa refa huyo, hajui kwanini aliulizwa maswali mengi juu ya kundi la kigaidi la Al-Shabab lililoko Somalia.

Related articles

Recent articles