33.2 C
New York

Petit afichua Enzo kuondoka Chelsea

Published:

LONDON, Uingereza

LEJENDARI wa Chelsea, Emmanuel Petit, amefunguka kuwa mshambuliaji Enzo Fernandez ni miongoni mwa mastaa wanaopaswa kuondoka Chelsea baada ya ujio wa kocha raia wa Hispania, Xabi Alonso.

Petit, raia wa Ufaransa aliyewahi kupita Arsenal, anaamini Enzo raia wa Argentina amechoka kuishi katika klabu hiyo ya Magharibi mwa Jiji la London.

“Enzo Fernandez anapaswa kuondoka, huwezi kumfurahisha mchezaji anayetaka kuondoka. Alishasema anataka kuondoka, akatozwa faini. Ni wazi hataki kubaki,” amesema.

Katika hatua nyingine, mkongwe huyo amefunguka kuwa haitashangaza kuona Enzo akijiunga na vigogo wa La Liga na soka la Hispania kwa ujumla, Real Madrid.

“Ni wazi anawindwa na Real Madrid ambayo inahaha kutafuta kiungo mpya. Sitoshangaa kuona akiondoka na kutimkia Real Madrid,” amesisitiza Petit.

Related articles

Recent articles