GILGIL, Kenya
MOTO ambao chanzo chake hakijafahamika umeripotiwa kusababisha vifo vya watu 16, wengi wao wakiwa ni wanafunzi, katika shule ya bweni ya Sekondari ya Wasichana ya Utumishi mjini Gilgil.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la AFP, mbali ya 16 waliopoteza maisha, wengine 73 wamejeruhiwa na wamelazwa hospitali kwa matibabu.
Taarifa ya polisi imeeleza kuwa uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha ajali hiyo ya moto ilipotokea mapema leo Mei 28, 2026.
Matukio ya moto katika shule za bweni si mageni nchini Kenya, mengi yakisabahisha na changamoto ya hitilafu ya umeme.
Itakumbukwa kuwa tukio kubwa zaidi ni lile la mwaka 2001, ambapo wanafunzi 67 walipoteza maisha katika Jimbo la Machakos.
Mwaka 2024, wanafunzi 21 waliteketea kwa moto, tukio lililosababisha Rais William Ruto kutangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa.


