VISA vya maambukizi ya ugonjwa wa Ebola vineripotiwa kuongezeka na kuiweka kwenye hali mbaya sekta ya afya chini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Takwimu rasmi za Serikali zinaonesha kuwa Ebola imesababisha vifo 160, huku maambukizi ya sasa yakifikia 670.
Aidha, mamlaka za DRC zimeeleza kuwa kasi ya maambukizi imeshuhudiwa zaidi katika maeneo ya Mashariki, ikiwamo mjini Bunia.
Hali hiyo imesababisha kutangazwa kwa Hali ya hatari, sambamba na kuzuiwa kwa mikusanyiko ya watu ili kudhibiti kasi ya maambukizi.
“Katika kila kituo cha kupima mizigo, kila lango la kuingilia nchini, kuna zoezi la upimaji, pamoja na utaratibu wa kuosha mikono,” amesema mmoja ya wataalamu wa afya, Aime Prospere.