Na Hassan Mwasha, Gazetini
BAADA ya kukosekana kwa misimu miwili mfululizo, safari hii Mbeya City bado inapitia wakati ngumu msimu huu wa Ligi Kuu Bara na hatari ni kubwa kwa timu hiyo kurudi ilikotoka (Championship).
Mbeya City iliyopanda msimu wa 2013-14, ilishuka daraja msimu wa 2023-24 baada ya miaka 10 mfululizo ya ushiriki wake kwenye mikikimikiki ya Ligi Kuu Bara.
Msimu huu, ikiwa katika nafasi ya 14 kwenye msimamo wenye timu 16 zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu wa 2025-26, ‘Wagonga Nyundo’ wana pointi 21 kati ya 69 walizopaswa kuwa nazo baada ya mechi 23
Katika mechi hizo, wakali hao wa jijini Mbeya wameshinda tano, sare sita na kufungwa 13, wakati huo pia wakiwa na mabao ya kufunga 18 na kufungwa 34.
Mwenendo huo usioridhisha unaifanya Mbeya City kuwa moja ya timu nne zilizo kwenye mstari mwekundu wa kuangukia aidha ‘play-off’ au kushuka daraja moja kwa moja.
Katika timu nne hizo, Namungo wako nafasi ya 13 wakiwa na pointi 24, Mbeya City wanafuata (21), kisha Tanzania Prisons (17) na KMC (9). Kufikia hatua hii, timu zote hizo ziko hatarini.
Je, hali itakuaje kwa Mbeya City kufikia mwishoni mwa msimu? Mechi sana zilizopo zitabadilisha upepo na kuwabakiza Ligi Kuu au zitakamilisha safar yao ya kurudi Championship?


