TEHRAN, Iran
WANAUME wawili nchini Iran wamekumbana na adhabu ya kunyongwa baada ya kubainika kujihusisha na upinzani dhidi ya Serikali.
Wawili hao waligundulika kuwa sehemu ya ‘People’s Mujahedin of Iran (MEK), ambacho ni kikundi cha upinzani kilichopigwa marufuku nchini humo.
MEK kimepigwa marufuku tangu miaka ya 1980 kikitajwa kuwa ni kikundi cha kigaidi, sifa ambayo pia inafahamika mbele ya Marekani na Umoja wa Ulaya (EU).
Sasa, tovuti ya Mahakama Kuu ndiyo iliyothibitisha kunyongwa kwa Akbar Daneshvarkar na Mohammad Taghavi-Sangdehi.
“Baada ya uthibitisho na ushahidi wa hukumu ya Mahakama Kuu, Akbar Daneshvarkar na Mohammad Taghavi-Sangdehi wamenyongwa leo asubuhi (Machi 30, 2026).
Kwa mujibu wa taarifa ya Mahakama, wanaume hao walijihusisha na vitendo vya maandamano na ugaidi.
Aidha, taarifa ikaongeza kuwa watu hao walipofanyiwa upekuzi, walikutwa na silaha kwenye makazi yao.


