6.4 C
New York

Sinner atinga fainali Miami Open

Published:

MIAMI, Marekani

NYOTA anayeshika nafasi ya pili kwa ubora duniani, Jannik Sinner, ameingia fainali ya michuano ya Miami Open baada ya kumtandika Alexander Zverev.

Sinner ameshinda mechi yake ya saba mfululizo dhidi ya Zverev na hii inakuwa mara ya nne kuingia fainali ya Miami Open.

Muitalia huyo amepata ushindi wa seti 6-3 7-6 (7-4) na sasa anajiandaa kukabiliana na raia wa Jamhuri ya Czech, Jiri Lehecka.

Kwa upande wake, Lehecka ametia mguu fainali baada ya ushindi wake wa seti 6-2 6-2 dhidi ya mkali raia wa Ufaransa, Arthur Fils, katika mchezo uliotumia dakika 75 kumalizika.

Endapo atashinda, basi litakuwa ni taji lake la pili la Miami Open kwa Sinner ndani ya miaka mitatu ya hivi karibuni.

Ikumbukwe, Sinner ambaye pia ni bingwa mtetezi wa Wimbledon, alitwaa taji la Indian Wells kwa kumfunga Zverev wiki chache zilizopita.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img