RIYADH, Saudi Arabia
SUPASTAA wa Al Nassr ya Ligi Kuu ya soka ya Saudi Arabia, Cristiano Ronaldo, ameondoka nchini humo usiku wa manane akikimbia mashambulizi ya Iran.
Iran imeshambulia ubalozi wa Marekani ulioko mjini Riyadh, Saudia. Ni baada ya Taifa hilo la Kiarabu kushambuliwa na vikosi vya Marekani na Israel.
Kuhusu Ronaldo, ambaye ni nahodha wa Al Nassr, aliondoka Saudia usiku wa jana Marchi 2, 2026 alitumia ndege yake binafsi.
‘CR7’ mwenye umri wa miaka 41, ametimkia mjini Madrid, Hispania, na ndege aliyotumia ni ile aliyoinunua kwa Pauni milioni 61.
Kwa mujibu wa taarifa, ndege hiyo aina ya Bombardier Global Express ilitumia saa 7 kumfikisha Madrid.


