Na mwandishi wetu, Gazetini
WACHAMBUZI wa siasa za kimataifa nchini Nigeria wanadhani nchi yao inaweza kufuata baada ya kile kilichoikuta Iran.
Marekani kwa kushirikiana na washirika wake wakubwa, Israel, zimeanzisha mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Iran.
Kwa mujibu wa Profesa wa Tafiti kutoka Chuo cha Mahusiano ya Kimataifa cha Nigeria, siasa za ulimwengu zimefikia hatua ya wababe (mataifa makubwa) kuvamia wanyonge (mataifa madogo).
Akitumia takwimu katika hoja hiyo, Profesa huyo amesema Marekani pekee imeshavamia kijeshi mataifa madogo zaidi ya 50 duniani kote.
Otubanjo ameongeza kuwa vita kwa sasa ni biashara kuwa duniani, ambapo mataifa makubwa yanavitumia kuuza silaha.
“Wanataka vita kwa sababu wanataka kuuza silaha zao. Katika hilo, Marekani ni mnufaikaji mkubwa. Ukiacha Marekani, Trump ananufaika mno na vita,” anasema.
Anasisitiza kuwa baada ya Iran, mataifa yaliyo hatarini kuingia kwenye mkono wa Iran ni Nigeria, Cuba na Afrika Kusini.


