16.3 C
New York

Museveni awapa somo vijana Uganda

Published:

KAMPALA, Uganda

RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni, amewataka vijana nchini humo kuacha kupoteza muda na nguvu kubwa kwenye ushabiki wa soka la Ulaya.

Na badala yake, watumie nguvu na muda huo kutafuta njia za kupata fedha na kujinasua kwenye umasikini.

Museveni, akiendelea kuwapa somo, amesema utajiri hupatikani kwa uzalishaji na si starehe za muda mfupi.

“Soko haliwezi kuwa na maana ikiwa huzalishi bidha au hutoi huduma ya kuuza. Hapo ndipo tunapopaswa kuanzia,” amesema.

Badala ya kupoteza muda kwenye mijadala ya soka la Ulaya, Museveni amewashauri vijana kujikita katika kilimo, utalii na sanaa ili kujiingizia kipato.

Aidha, amesema inashangaza kuona vijana hawajitokezi kuchangamkia miradi ya uwezeshaji kiuchumi, ikiwamo mikopo, inayoratibiwa na Serikali.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img