16.3 C
New York

Marekani, Israel zamuua Ali Khamenei

Published:

TEHRAN, Iran

NI rasmi sasa, kwamba kiongozi wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, ameuawa na vikosi vya Marekani vinavyoshirikiana na Israel.

Marekani na washirika wake, Israel, wameanzisha mashambulizi ya makombora nchini Iran kwa madai ya nchi hiyo kugoma kuacha uzalishaji wa silaha za nyuklia.

Sasa, Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema Ali Khamenei ameuawa akiwa ofisini kwake asubuhi ya jana Februari 28, 2026.

Akimzungumzia, Trump alimtaja Ali Khamenei kuwa ni mmoja ya viongozi waovu kuwahi kutokea katika siasa za ulimwengu.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari, likiwamo Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), viongozi wa Iran takribani 40 waliuawa pia.

Katika taarifa yake, Israel imekiri kuua viongozi wa Serikali ya Iran wakati wa shambulizi la anga lililohitimisha maisha ya Ali Khamenei.

Zipo taarifa kuwa tayari mashambulizi ya Marekani na Israel yameshasababisha vifo vya watu zaidi ya 200 nchini Iran.

Tukio la kusikitisha zaidi lililoripotiwa ni lile la mashambulizi hayo kuisambaratisha shule iliyokuwa na takribani 180.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img