5.7 C
New York

Vilevi vinavyotumiwa na vijana wengi Marekani

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

KWA miaka mingi, matumizi ya vilevi yamekuwa yakitafsiriwa kuwa ni mtindo wa kisasa wa maisha ya vijana wengi duniani kote.

Licha ya kutokuwapo kwa utafiti, tunaweza kukubaliana kuwa katika jamii nyingi, ni vijana wachache tu waliofanikiwa kuepuka aina yoyote ya kilevi.

Ni kutokana na hilo, utafiti wa Chuo Kikuu cha Michigani cha Marekani umeshawishika kufahamu aina ya vilevi vinavyotumiwa zaidi na vijana nchini humo.

Katika hilo, utafiti huo ulihusisha vijana wenye umri kati ya miaka 19 hadi 30, ambao waliulizwa juu ya vilevi walivyotumia zaidi kwa mwaka jana.

Kupitia utafiti huo, walibaini kuwa asilimia 81 ya vijana hao walikiri kutumia pombe ndani ya kipindi hicho cha miezi 12.

Kupitia mahojiano yao na vijana hao, watafiti walibaini kuwa asilimia 25 ya vijana walikuwa wakitumia pombe kila siku.

Kama hiyo haitoshi, asilimia 41 walikiri kutumia kilevi aina ya bangi, idadi ambayo ni kubwa mara mbili, ukilinganisha na ilivyokuwa mwanzoni mwa miaka ya 2010.

Aidha, asilimia 11 ya vijana hao waliohojiwa na watafiti wa Chuo Kikuu cha Michigani walikiri kuvuta bangi mara 20 ndani ya siku 30.

Kwa upande mwingine, uvutaji wa sigara za kawaida umeshuka, ambapo ni asilimia 18 pekee ya vijana waliosema walivuta sigara mwaka 2024.

Na badala yake, asilimia 26 walikiri kuwa ni watumiaji wakubwa wa shisha, ambayo inatajwa kuchukua nafasi ya sigara za kawaida miongoni mwa vijana.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img