9 C
New York

Ukraine, Urusi hakijaeleweka mazungumzo ya kumaliza vita

Published:

GENEVA, Uswis

MAZUNGUMZO yanayoendelea kati ya Ukraine, Urusi na Marekani mjini Geneva yamemalizika, ingawa hakuna mwafaka uliofikiwa.

Marekani ikiwa msuluhishi, inajaribu kumaliza vita vilivyodumu kwa miaka kadhaa kati ya majirani hao wa Ulaya ya Mashariki.

Mazungumzo hayo yaliyoanza juzi yaliendelea leo Februari 18, 2026 lakini yalidumu kwa saa mbili pekee.

Awali, Mjumbe wa Marekani katika mazungumzo, Steve Witkoff, alionesha matumaini ya pande mbili hizo kufikia makubaliano ya kusitisha vita.

Hata hivyo, mwakilishi wa Urusi na Volodymyr Zelensky wa Ukraine wamesema kuna ugumu katika makubaliano.

Baada ya mazungumzo hayo, mwakilishi wa Urusi, Vladimir Medinsky, alikutana na kufanya mazungumzo ya dakika 90 na Zelensky.

Lakini, bado kile kilichozungumzwa katika kikao chao hakijawekwa wazi, kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC).

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img