8 C
New York

Utafiti: Sekta ya elimu bado janga Afrika

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

UTAFITI wa Taasisi ya Afrobarometer Pan-Africa umezitaka Serikali barani Afrika kuwekeza jitihada za kutosha katika elimu, ukiitaja sekta hiyo kuwa ni janga barani humo.

Katika utafiti uliohusisha watu 50,961 kutoka mataifa 53 waliohojiwa na Afrobarometer Pan-Africa, wengi (zaidi ya asilimia 50) walieleza kutokuridhishwa na mfumo wa elimu uliopo Afrika.

Wanawake, wakazi wa maeneo ya vijijini na wananchi wa kipato cha chini, kwa mujibu wa utafiti huo, bado wameonekana kuwa na kiwango kidogo cha elimu.

Kwamba ni wawili tu kati ya watu 10 wa makundi hayo matatu waliofanikiwa walau kuvuka kiwango cha elimu ya sekondari.

Aidha, asilimia 39 wameishia sekondari, asilimia 26 walikwamia elimu ya msingi, huku asilimia 16 wakiwa hawajawahi kwenda shule kabisa.

Wakati huo huo, changamoto ya ubaguzi wa kijinsia katika kupata elimu nayo imejitokeza kwa kiwango cha kushitua.

Mathalan, kupitia utafiti huo wa Afrobarometer Pan-Africa, familia nyingi zimeonekana kuwapa kuwapuuza mabinti linapokuja suala la kusomesha watoto.

Kama hiyo haitoshi, watu watatu kati ya 10 katika utafiti huo walikiri kuwa watoto wa kike hukumbana na ubaguzi na unyanyasaji wa kijinsia hata kutoka kwa waalimu wao.

Matokeo ya utafiti yanazitaja Gabon (71%) na Cameroon (55%) kuwa ndiko vitendo vya unyanyasaji vimejitokeza zaidi, tofauti na ilivyo kwa Madagascar (9%) na Mauritius (2%).

Lakini, licha ya changamoto zilizopo, wengi waliohojiwa, ambao wanafikia asilimia 81, wanaunga mkono sera ya wanafunzi waliopata ujauzito kuendelea na masomo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img