30.9 C
New York

Sare zaitibulia Simba, yapoteza rekodi ya msimu uliopita

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

KAMA kuna jambo wanaloweza kujilaumu Simba endapo wataikosa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, basi ni sare nyingi walizovuna katika mechi zao.

Kufikia hatua hii ya msimu wa 2025-26, Wekundu wa Msimbazi wamekusanya sare saba, sawa na asilimia 28 ya michezo 25 waliyocheza nyumbani na ugenini.

Kwa idadi hiyo, ni wazi Simba wameiharibu rekodi yao ya msimu uliopita, ambao waliumaliza wakiwa na sare tatu pekee, sawa na asilimia 10 ya mechi 30 walizocheza.

Kutokana na wingi huo wa sare, hesabu zinaonesha kuwa Simba haitoweza kufikia asilimia 90 ya ushindi wa mechi zake za msimu uliopita, ambapo ilishinda mara 27 katika michezo 30.

Kwa sasa, Simba ya kocha raia wa Afrika Kusini, Steve Barker, imeshinda mara 17, sawa na asilimia 68 ya mechi zake 25. Imefungwa mechi moja pekee.

Hivyo, kwa hesabu za kawaida, hata kama watapata matokeo chanya (ushindi) katika mechi tano zilizobaki, watamaliza msimu wakiwa wameshinda mara 22.

Wekundu wa Msimbazi wana pointi 58 wakishika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, wakiipumulia Yanga inayoongoza kwa tofauti ya pointi mbili.

Related articles

Recent articles