Na mwandishi wetu, Gazetini
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga, wako kileleni mwa msimamo wakiwa na pointi 60 lakini wamebakiza mechi tano, ambazo kama watashinda zote, basi watamaliza msimu huu wakiwa na pointi 75.
Hata hivyo, ni pointi chache zaidi kwa Yanga kuwa nazo, ikilinganishwa na ilivyofanya misimu mitatu mfululizo ya hivi karibuni (2024-25, 2023-24 na 2023-22).
Iko hivi; takwimu zinaonesha kuwa mara zote hizo Yanga ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu ikiwa na pointi zaidi ya 75 baada ya kucheza mechi 30.
Msimu uliopita, 2024-25, ‘Timu ya Wananchi’ ilibeba taji ikiwa na pointi 82. Msimu wa nyuma yake, 2023-24, ilikusanya pointi 80, na msimu wa 2023-22 ilipata pointi 78.
Hivyo, mara ya mwisho kwa Wanajangwani kutwaa ubingwa wa Ligi wakiwa na pointi chini ya 78 ni msimu wa 2022-21 (pointi 74).


