5.7 C
New York

Aliyekimbia polisi miaka 16 akamatwa, Olimpiki yamponza

Published:

MILAN, Italia

MWANAUME raia wa Slovakia ameangukia mikononi mwa polisi mjini Milan, Italia, baada ya miaka 16 ya kujificha akikwepa kukamatwa.

Mtu huyo anayetajwa kuwa na umri wa miaka 44, ameponza na michuano ya Olimpiki inayoendelea mjini Milan.

Iko hivi; baada ya miaka mingi ya kuwakimbia polisi, alifika Milan hivi karibuni, akivutwa na mapenzi yake katika mchezo wa ‘hockey’.

Hata hivyo, kumbe tayari jina lake lilishawekwa kwenye orodha ya wezi waliotakiwa kukamatwa kwa agizo la waendesha mashitaka wa Milan.

Safari hii, polisi walishazinasa taarifa zake za kuja kushuhudia michuano ya Olimpiki, hivyo ikawa rahisi kumfuatilia na hatimaye kumdaka akiwa kwenye nyumba ya wageni aliyofikia.

Kwa sasa, ameswekwa katika Gereza la San Vittore na anatarajiwa kuwa hapo kwa kipindi cha miezi 11 na wiki moja kwa matukio ya wizi aliyofanya mwaka 2010.

Hivyo, jamaa huyo alishindwa kwenda uwanjani kuitazama timu ya taifa ya Slovakia ya mchezo wa Hockey ikiifunga Finland.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img