5.7 C
New York

Polisi: Aliyeua watu nane ana changamoto ya afya ya akili

Published:

TORONTO, Canada

POLISI nchini Canada wamebaini kuwa mshukiwa wa mauaji ya watu nane, ambaye ni mwanamke, ana changamoto ya afya ya akili.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 18 alitekeleza mauaji hayo kwa kufyatua risasi hovyo katika shule moja mjini Tumbler Ridge.

Mmoja kati ya watu hao ni mwalimu, wakati watano ni wanafunzi wenye umri kati ya miaka 12 na 13.

Kabla ya tukio hilo, taarifa zinaeleza kuwa mshukiwa huyo alitekeleza mauaji katika familia yake, ambapo alimuua mama na mdogo wake wa kiume mwenye umri wa miaka 11.

Baada ya uchunguzi, imebainika kuwa mshukiwa huyo aliwahi kutembelewa mara kadhaa na maofisa wa polisi kutokana na changamoto ya afya ya akili.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img