6.4 C
New York

Kim Kardashian na wanaume 14 aliotoka nao kimapenzi

Published:

LOS ANGELES, Marekani

STORI inayobamba kwa sasa kwenye tasnia ya burudani nchini Marekani ni hii ya mrembo Kim Kardashian kuanika penzi lake jipya na staa wa mchezo wa mashindano ya magari, Lewis Hamilton.

Kim aliwahi kuwa mke wa rapa tajiri, Kanye West, ambaye alidumu naye kwenye ndoa kwa miaka saba kabla ya kila mmoja kushika njia yake mwaka 2022.

Hata hivyo, Hamilton na Kanye si wanaume pekee waliowahi kutoka na bibiye huyo anayetokea familia maarufu ya Kardashian.

Damon Thomas

Akiwa na umri wa miaka 19, Kim aliingia kwenye uhusiano na prodyuza wa muziki, Damon. Wawili hao walifunga ndoa lakini waliachana mwaka 2004.

Kwa mujibu wa ripoti za wakati huo, chanzo cha kuachana kwao ni Kim ‘kuchepuka’ na mshikaji aitwaye Ray J. Jamaa alidai kuwa bibiye huyo ndiye aliyemshawishi wamsaliti Damon.

Ray J

Alikutana na Kim mwaka 2025, wakati huo Kim alipokuwa mfanyakazi wa mwanamuziki maarufu wa R&B, Brandy, ambaye pia ni dada wa mshikaji huyo.

Walipoachana, ndipo Ray J alipofunguka kuwa Kim alimshawishi watoke kimapenzi, licha ya kwamba alikuwa mke wa mtu (Damon).

Nick Lachey

Baada ya kuachana na staa wa muziki, Jessica Simpson, Nick aliangukia kwa Kim. Walinaswa mara kadhaa na kamera za mapaparazi wakifurahia maisha katika hoteli za kifahari mjini Los Angeles.

Hata hivyo, penzi lao halikudumu, ingawa chanzo cha wawili hao kuachana hakikuwekwa wazi. Kila mtu akaanza maisha yake mapya.

Nick Cannon

Mwigizaji huyo anafahamika zaidi kwa uhusiano wake na bibiye mwenye jina kubwa katika soko la muziki nchini Marekani, Maria Carey.

Pia, Cannon aliwahi kuwa na Kim, ingawa walishindwana ndani ya muda mfupi tu. Waliachana mwaka 2007.

Reggie Bush

Kim na Bush walianza kuwa na uhusiano mwaka 2007. Penzi lao kilikuwa na migogoro mingi ya kuachana na kurudiana, kabla ya kutemana moja kwa moja mwaka 2010.

Lakini, kwa mujibu wa maparazi, Bush aliendelea kumtumia meseji Kim hata baada ya kumuoa mrembo mwingine aitwaye Kris Humphries.

Cristiano Ronaldo

Mwaka 2010, Jarida maarufu la Page liliibua stori ya Kim na Cristiano Ronaldo kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi. Ni baada ya Kim kuonekana mjini Madrid.

Wakati huo, Ronaldo alikuwa mchezaji wa Real Madrid. Ikaelezwa kuwa wawili hao walikuwa na wakati mzuri ndani ya hoteli ya kifahari ya Beverly Hills.

Miles Austin

Ilikuwa Julai, 2010, ambapo Jarida la Page lilidai kuwa Kim na mshikaji huyo wameonekana usiku katika moja ya hoteli za bei mbaya mjini New York.

Hata hivyo, vyanzo vingine vya habari vilikanusha na kusema wawili hao ni marafiki, hivyo hakuna uhusiano wa kimapenzi.

Michael Copon

Oktoba, 2010, iliripotiwa kuwa Kim ameangukia kwenye penzi la Copon. Moja ya magazeti yaliandika ‘Kim anatoka na Copon’.

Baadaye, Copon aliibuka na kukanusha. Pia, Jarida la Page lilieleza kuwa hakuna kinachoendelea kati ya Kim na mshikaji huyo.

John Mayer

Ripoti za Mayer na Kim kuwa wapenzi zikiibuka mwaka 2010 pia. Walikutana na kufurahia usiku mmoja wakiwa na marafiki zao, kwa mujibu wa Jarida la Page.

Baadaye, mtandao maarufu wa habari za mastaa ulidai kuwa Kim na Mayer walikutana tena mara kadhaa baada ya siku hiyo ya kujumuhika na marafiki zao.

Gabriel Aubrey

Novemba, 2010, Jarida la Page liliibua stori ya Aubrey kuwa na Kim. Picha zikavuja zikiwaonesha wawili hao wakiwa pamoja maeneo mbalimbali.

Hata hivyo, kama ilivyokuwa kwenye mahusiano mengine yaliyopita, Kim hakudumu na mshikaji wake huyo.

Kris Humphries

Baada ya miezi sita ya uchumba, Humphries alifunga ndoa na Kim mwaka 2011. Ni ndoa ambayo haa hivyo ilidumu kwa siku 72 tu. Kim akaomba talaka.

Kwa mujibu wa Kim, ndoa ilikuwa tamu wakati wa fungate tu, kisha mambo yakaenda vibaya na kila mmoja kuona inatosha.

Kanye West

Baada ya mwaka mmoja wa kuwa kwenye uhusiano, Kim na Kanye walipata mtoto wao wa kwanza Juni, 2013, ambaye anaitwa North.

Hatimaye, walifunga ndoa Mei, 2014 mjini Florence, Italia. Hata hivyo, ndoa ilivunjika rasmi mwaka 2022 wakiwa tayari wana watoto wengine wanne (Saint, Chicago na Psalm).

Pete Davidson

Alipoachana na Kanye, Kim alianzisha uhusiano na staa wa vichekesho, Davidson. Mshikaji alionekana ni mwenye furaha alipohudhuria sherehe ya ‘birthday’ ya Kim alipotimiza umri wa miaka 28.

Hata hivyo, Kim na Davidson waliachana Agosti, 2022 wakiwa wamedumu kwenye uhusiano kwa miezi tisa pekee.

Hamilton

Wamekuwa wakifahamiana kwa miaka zaidi ya 10. Kim akiwa mtangazaji maarufu wa vipindi vya runinga, huku Lewis akiwa staa wa mbio za magari kupitia michuano ya Formula One.

Hivi karibuni, Kim alitumia ndege yake binafsi kusafiri kutoka Marekani hadi Uingereza, ikielezwa kuwa alikwenda kumtembelea Hamilton.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img