27.3 C
New York

Mastaa hawa wameyakataa mataifa waliyozaliwa Kombe la Dunia 2026

Published:

MEXICO CITY Mexico

FAINALI za Kombe la Dunia za mwaka huu (2026) zimeshuhudia idadi kubwa zaidi kuwahi kutokea ya wachezaji walioyapa kisogo mataifa waliyozaliwa.

Takwimu zinaonesha kuwa robo ya wachezaji walioko Kombe la Dunia wanatumikia mataifa tofauti na walikozaliwa na wengine wameyafunga walipokutana nayo.

Morocco iliandika historia mpya baada ya ‘firts elevn’ yake dhidi ya Brazil kutokuwa na hata mchezaji mmoja aliyezaliwa nchini humo.

Makala haya yanakukumbusha baadhi tu ya wachezaji waliopo Kombe la Dunia 2026, ambao wamechagua kuyatema mataifa waliyozaliwa.

IBRAHIM MBAYE

Alizaliwa Ufaransa lakini yuko na kikosi cha timu ya soka ya Taifa ya Senegal. Mbaye anayekipiga PSG, aliifunga Ufaransa katika mchezo ambao hata hivyo Senegal ilitandikwa mabao 3-1.

BREEL EMBOLO

Ni mshambuliaji mzaliwa wa Cameroon lakini amechagua kuiwakilisha timu ya soka ya Taifa ya Uswis. Katika fainali za Kombe la Dunia za 2022, Embolo alifunga bao alipokutana na Cameroon.

MICHAEL OLIS

Winga wa daraja la juu katika kikosi cha timu ya soka ya Taifa ya Ufaransa. Olise amechagua kuipa kisogo England, ambako ndiko alikozaliwa katika Jiji la London. Ufaransa ndiko anakotokea mama yake.

ANTONEE ROBINSON

Ni miongoni mwa mastaa wengi waliozaliwa nje ya Marekani lakini wameichagua timu hiyo. Robinson alizaliwa England lakini ameipenda Marekani anakotoka baba yake.

ACHRAF HAKIMI

Beki wa kulia, ambaye pia ndiye nahodha wa timu ya soka ya Taifa ya Morocco. Hakimi angeweza kuitumikia Hispania alikozaliwa lakini amelichagua Taifa hilo la Afrika ya Kaskazini. Ni kama ilivyo kwa Hakim Ziyech.

Related articles

Recent articles