MUNICH, Ujerumani
KOCHA wa zamani wa Liverpool, Jurgen Klopp, amewataja Lionel Messi na Cristiano Ronaldo kuwa ndiyo wachezaji bora duniani kwa sasa.
Klopp amesema siyo ishu ya ubora wao, bali pia namna nyota hao walivyoweza kudumu kwa muda mrefu kwenye kiwango cha juu.
“Nikiwa kama shabiki wa kawaida, inanichaganya kwa namna walivyotawala kwa miaka 10 hadi 15 iliyopita,” amesema.
“Baada ya mechi ya kwanza, ambapo Cristiano Ronaldo alikosolewa, inaweza kuona alivyorudi. Unazungumzia mchezaji mwenye umri wa miaka 41,” amesema Klopp.
Messi amefikisha mabao 18 kwenye historia ya Kombe la Dunia, wakati Ronaldo ana 10.


