MEXICO CITY, Mexico
KATIKA hatua ya 32 Bora ya msimu huu wa Kombe la Dunia, timu ya soka ya Taifa ya Uholanzi itakuwa na kibarua kigumu mbele ya vigogo wa soka la Afrika, Morocco.
Uholanzi imetinga 32 Bora ikiwa imemaliza kileleni mwa Kundi F baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Tunisia.
Kwa upande wao, Morocco waliingia hatua hii kwa ushindi mnono wa mabao 4-2 dhidi ya Haiti.
Mchezo mwingine mkali wa hatua hiyo ya 32 Bora utazikutanisha Brazil na Japan.
Vilevile, upo mchezo utakaozikutanisha Marekani na Bosnia, wakati Afrika Kusini itakwaana na Canada.


