9.2 C
New York

Beki auawa na mdogo wake wakigombea kiwanja

Published:

NAIROBI, Kenya

NI mlinzi wa Kakamega Homeboyz ya Ligi Kuu nchini Kenya, Silas Abungana, ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 25.

Abungana (25), ameiaga dunia baada ya kupigwa na mdogo wake wakati wa ugomvi ambao chanzo chake kimetajwa kuwa ni kugombea kiwanja.

Chanzo cha habari hiyo kimedai kuwa Abungana alipigwa na chuma kichwani na kukimbizwa Hospitali ya Jimbo la Kakamega County.

“Ni huzuni kuona tumepoteza mchezaji chipukizi. Alishaanza kuzoeana na wenzake baada ya kusajiliwa akitokea Shabana mwanzoni mwa msimu huu,” kimeeleza chanzo hicho.

Kwa upande wake, mke wa mchezaji huyo, Mary Wandera, amesema kifo cha Abungana kimeacha pengo si tu kwa tasnia ya michezo, bali pia kwa familia yake.

Wakati huo huo, klabu yake ya Kakamega Homeboyz imeeleza kusikitishwa na kifo cha mchezaji wake huyo. “Klabu ya soka ya Kakamega Homeboyz imesikitishwa na kifo cha Silas Abungana.”

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img